Print 

UKIUSHI KAMA ELEMENTI YA KIMTINDO KATIKA BAADHI YA RIWAYA ZA KEN WALIBORA

Mercy Moraa Motanya - Chuo Kikuu cha Kabianga, Kenya

Emmanuel Kisurulia - Chuo Kikuu cha Kabianga, Kenya

Salim Sawe - Chuo Kikuu cha Kabianga, Kenya


IKISIRI

Makala haya ni uchanganuzi wa ukiushi kama elementi ya mtindo kwenye riwaya nne za Kiswahili zilizoandikwa na Ken Walibora kutumia mkabala wa kiisimu. Isimu ni taaluma inayochunguza lugha kwa kuzingatia taratibu za kisayansi. Uchanganuzi wa data ambao ulitumiwa ni wa kimaelezo na uliongozwa na nadharia ya umitindo. Nadharia hii ina nguzo za kuchanganua kazi za fasihi kwa misingi ya kiisimu na hubainisha kanuni za kuelezea uteuzi uliofanywa na mwandishi katika matumizi yake ya lugha kuhusu mambo ya kijamii, utoaji na upokeaji wa maana, uhakiki wa kidiskosi na ule wa kifasihi. Lengo mahsusi ni kuchanganua aina za ukiushi katika riwaya nne za Ken Walibora. Sampuli iliteuliwa kimaksudi na data ilikusanywa kwa njia ya kusoma vitabu husika na kisha kudondoa mifano mwafaka na kuinakili kwa ajili ya kutoa maelezo kulingana na lengo la utafiti huu. Makala haya ni muhimu kwa kuwa yameweka wazi namna waandishi wa riwaya za Kiswahili wanavyotumia ukiushi kama elementi ya mtindo wa kiisimu ili kuwasilisha ujumbe wao katika kazi za fasihi.


Full Length Research (PDF Format)